IQNA

Muqawama

Jenerali Qaani ashiriki mazishi ya Shahidi Nilforoushan

11:58 - October 15, 2024
Habari ID: 3479596
IQNA-Brigedia Jenerali Ismael Qaani, Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ameshiriki katika mazishi ya Shahid Abbas Nilforoushan.

Mwili wa shahid Abbas Nilforoushan ambaye aliuawa kidhulma kwenye shambulio la kigaidi na kikatili lililofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Beirut, mji mkuu wa Lebanon, umewasili usiku wa kuamkia leo Jumanne katika Uwanja wa Ndege wa Mehrabad hapa Tehran.

Brigedia Jenerali Ismael Qaani, Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC  ameonekana akiwa kwenye kikao cha maombolezo kilichohudhuriwa na wakuu mbalimbali za kisiasa na kijeshi, watu wa familia ya shahid Nilforoushan na kadhalika.

Katika siku za hivi karibuni vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimekuwa vikieneza uvumi kuhusu Jenerali Qaani  na hivyo kuonekana kwake hadharani kumesambartisha uvumi uliokuwa unaenezwa.

Shahid Nilforoushan aliuawa kikatili tarehe 27 Septemba 2024, kusini mwa Beirut, mji mkuu wa Lebanon akiwa pamoja na Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchi hiyo.

Shahid Nilforoushan alikuwa mmoja wa shakhsia na makamanda muhimu sana wa Iran aliyeongoza operesheni nyingi za kuwasaidia Walebanon na Wapalestina katika kupambana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Aliisaidia sana kambi ya Muqawama katika mipango ya kijeshi na kidiplomasia na namna ya kukabiliana na jinai za Israel ndio maana utawala wa Kizayuni ulikuwa na chuki na uadui mkubwa na mwanamapambano huyo wa Kiislamu.

4242488

Habari zinazohusiana
captcha