Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa IRGC alitoa onyo hilo Jumatano, siku mbili baada ya jeshi la utawala haramu wa Israel kufanya mashambulizi ya anga katika mji huo wa Syria.
Hujuma hizo za Wazayuni usiku wa Jumatatu iliyopita zilipelekea watu 17 kuuawa shahidi, akiwemo Saeed Abyar, mshauri wa kijeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran. Watu wengine 15 wa walijeruhiwa.
Meja Jenerali Salami amesema mashambulizi na uvamizi wa utawala wa Kizayuni nchini Syria unakanyaga sheria za kimataifa, Hati ya Umoja wa Mataifa mbali na kuwa tishio kubwa kwa amani na uthabiti wa eneo la Asia Magharibi.
Amesema, "Watenda jinai wa Kizayuni wanaoua watoto wanapaswa kufahamu kuwa, watalipa gharama ya kumwaga damu za watu wasio na hatia katika jinai hii; wanapasa kusubiri jibu (la Iran)."
Kamanda Salami ameuhutubu utawala wa Kizayuni kwa kufanya jinai hiyo ya kutisha huko Halab na kusema: Mnapaswa kufahamu kuwa, mkitoa vitisho dhidi ya usalama wa Iran, tutakuwa na machaguo mengi.
Kabla ya Aleppo (Halab) kukabiliwa na mradi wa uasi ulioanza kutekelezwa na maadui mwaka 2011, ulichukuliwa kuwa mji mkuu wa kiuchumi wa Syria. Mji huo ulinawiri kiuchumi kabla ya maadui kuanza kutekeleza njama za kuiangusha serikali halali ya Rais Bashar al-Assad.
3488632