IQNA

Indhari ya Ayatullah Issa Qassim kuhusu matokeo mabaya ya kuanzisha uhusiano na Israel

20:38 - December 02, 2020
Habari ID: 3473414
TEHRAN (IQNA) - Mwanazuoni na kiongozi juu wa Kiislamu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Bahrain amesema kuwa, matokeo ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel yatakuwa hatari na yatasababisha majanga.

Ayatullah Issa Qassim ambaye pia ni Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain ameeleza kwamba, baadhi ya tawala za Kiarabu zilizoanzisha uhusiano wa kawaida na adui Mzayuni zimejitenga na wananchi wao na kukimbilia kwa Marekani na Israel na kukabidhi hatima ya mataifa yao mikononi mwa tawala hizo kandamizi.

Sheikh Issa Qassim ameongeza kusema kuwa, kudhalilika mataifa yaliyoanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel kumedhihirika haraka mno ikiwa ni muda mfupi tu baada ya viongozi wa mataifa hayo kutia saini makubaliano ya usaliti.

Baada ya Imarati na Bahrain kutangaza kuwa zimeafiki kuutambua rasmi utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, mnamo tarehe 15 Septemba, nchi hizo mbili za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi zilisaini rasmi mkataba wa kuanzisha uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia na utawala huo unaoikalia Quds tukufu kwa mabavu, katika hafla iliyofanyika Ikulu ya White House, mjini Washington na kuhudhuriwa na rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

3473295

captcha