IQNA

Rais Putin anukulu aya za Qur'ani katika 'Siku ya Umoja wa Kitaifa' Russia

20:51 - November 06, 2020
Habari ID: 3473334
TEHRAN (IQNA)- Kwa mujibu wa taarifa, Putin ameyasema hayo alipohutubu kwa njia ya video katika mjumuiko wa Siku ya Kitaifa ya Russia.

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Kiislamu, Kikrosti, Kiyahudi na Kibuddha.

Katika kikao hicho Rais wa Russia alisoma sehemu ya aya ya 23 ya Sura Ash-Shuraa ya Qur'ani Tukufu isemayo: " Sema: Sikuombeni malipo yoyote kwenu ila mapenzi katika kujikurubisha….". Aidha amenukulu aya ya 128 ya Sura An Nahl ya Qur'ani Tukufu  isemayo: "  Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na watendao mema."

Katika hotuba yake hiyo Putin pia alinukuku Taurati, Injili na kitabu kitukufu cha Mabudhha kuhusu umuhimu wa Amani na maelewano baina ya wafuasi wa dini na kaumu mbali mbali.

Rais wa Russia amebainisha masikitiko yake kutokana na watu ambao wanaeneza fitina na kuvunjia heshima wafuasi wa dini zingine kwa kisingizio cha uhuru wa maoni. Ametoa wito kwa viongozi wa kidini Russia kuzuia mifarakani ya kidini nchini humo.

3933524

captcha