IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Hafidh wa Iran kushirki Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Urusi

17:13 - October 21, 2024
Habari ID: 3479626
IQNA - Iran itashiriki katika mashindano yajayo ya kimataifa ya Qur'ani katika mji mkuu wa Urusi (Russia).

Mashindano ya 22 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Moscow yamepangwa kufanyika mapema mwezi ujao. Mohammad Rasoul Takbiri, mhifadhi wa Qur'ani nzima, ataiwakilisha Iran katika hafla hiyo ya kimataifa. Mwaka jana, Hossein Khani Bidgoli aliishindania Iran katika makala ya 21 ya shindano hilo na kumaliza mshindi wa pili huku waliokariri kutoka Urusi na India wakiwa wa kwanza na watatu mtawalia.

Imepangwa kuanzia Novemba 6-8, toleo la 22 litaandaliwa na Utawala wa Kiroho wa Waislamu wa Shirikisho la Urusi kwa msaada wa wizara ya Qatar ya Wakfu na masuala ya Kiislamu.

Wahifadhi Qur'ani kutoka zaidi ya nchi 30 watashiriki katika mashindano hayo. Maonyesho ya washindani yatafanyika katika Msikiti wa Jamia wa Moscow.

3490360

Habari zinazohusiana
captcha