IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi watunukiwa Tuzo ya Kwanza ya Qur'ani Tukufu ya BRICS huko Kazan

22:58 - July 27, 2024
Habari ID: 3479193
IQNA - Sherehe za kufunga Tuzo ya Qur'ani Tukufu ya BRICS zilifanyika siku ya Ijumaa huko Kazan katika Jamhuri ya Tatarstan nchini Russia huku washindi wa mashindano hayo wakitunukiwa.

Wagombea kutoka nchi 22, wakiwemo wanachama wa BRICS, walishiriki katika shindano hilo la kuhifadhi Qur’ani Tukufu lililoanza Jumatano.

Nafasi ya kwanza ilitolewa kwa Mohamed Samir Mohamed kutoka Bahrain.

Nafasi ya pili ilikwenda kwa Mohamed Abdelkarim Kamil Attiyah kutoka Misri, ambaye amehifadhi Quran licha ya kuzaliwa kipofu.

Omid Hosseininejad kutoka Iran alipata nafasi ya tatu.

Hafla hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Kiroho wa Waislamu wa Shirikisho la Russia, Baraza la Mufti wa Russia, na Chuo Kikuu cha Mohamed Bin Zayed (UAE), kwa msaada kutoka Jamhuri ya Tatarstan.

Jopo la majaji, lililojumuisha wataalamu mashuhuri wa Qur'ani kutoka Russia, Yemen, Bangladesh, Iran na Misri, lilitathmini mashindano hayo.

3489255

captcha