IQNA

Polisi Austria wakosolewa kwa kuwasumbua Waislamu

22:15 - November 17, 2020
Habari ID: 3473368
TEHRAN (IQNA)- Polisi nchini Austrai wamekosolewa vikali kwa kuwasumbua na kuwakera Waislamu ambao wamekuwa wakihujumu maeneo yao na kuwauliza maswali ya dharau.

Kwa mujibu wa asasi moja wa kiraia, katika oparehseni iliyotajwa kuwa ni ‘dhidi ya ugaidi’ polisi Austrai walishambulia nyumba 60 za wasomi na wanaharakati Waislamu mnamo Novemba 9.

Katika oparesheni hiyo watu kadhaa walitiwa mbaroni wakiwa ni washukiwa wa ugaidi.

Asasi ya kiraia inayojulikana kama Jukwaa la Mshikamano wa Palestina Austria (Palästina Solidarität Österreich), polisi w alishambulia nyumba za Waislamu hao saa 11 alfajiri ambapo wakaazi, wakiwmeo watoto wadogo walilazimishw akutoka nje ya nyumba bila ya kuruhusiwa kuvaa mavazi ya nje wakati huu wa baridi kali. Waislamu hao waliulizwa maswali yasiyowahusu huku watoto wakiulizwa ‘baba huficha wapi pesa’, na iwapo wao huswali msikiti au kutekeleza ibada nyinginezo nyumbani.

Austria inakosolewa kwa kugeuka na kuwa kituo cha sera za chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya.

3473154

Kishikizo: austria ، waislamu ، polisi
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha