IQNA

Mashindano ya Qur’ani ya Dubai yaendelea

20:05 - November 20, 2020
Habari ID: 3473377
TEHRAN (IQNA) – Duru ya 14 ya Mashindano ya Qur’ani ya Dubai nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inaendelea katika mji huo.

Mashindano hayo ya kila mwaka huandaliwa na Idara ya  Masuala ya Kiislamu na Misaada Dubai na mwaka huu inafanyika kwa njia ya intaneti kutokana na kuenea ugonjwa ambukizi wa corona.

Kuna washiriki 97 katika mashaindano ya mwaka huu ambayo yanamalizika Novemba 25.

Afisa mwandamizi wa mashindano Hamd Ahmed al – Muhayri amesema mashindano hayo ya mwaka huu yanafanyika katika kategoria sita. Washiriki wametoka kutoka katika taasisi mbali mbali za Qur’ani nchini UAE.

Nara na kauli mbiu ya mwaka hii ni aya ya 26 ya Surah al Mutaffifin ya Qur’ani Tukufu isemayo: “Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana.”

Baada ya kuibuka ugonjwa ambukizi wa corona Februari mwaka huu, mijimuiko ya kiutamaduni, kidini, na kisiasa nchini UAE imepigwa marufuku.

3936190

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha