IQNA

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Dubai watangazwa

20:01 - April 25, 2021
Habari ID: 3473849
TEHRAN (IQNA)- Washindi wa Mashindano ya 24 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani ya Dubai wametangazwa na kutunukiwa zawadi.

Sherehe ya kuwatunuku zawadi imefanyika Jumamosi usiku ambapo majaji walimtangaza Muhammad Abu Qassim wa Syria ametangazwa kuwa mshindi wa duru hii.

Abdul Ghani Yahya wa Marekani na Muzzamil Muhammad wa Sudan wamechukua nafasi ya pili nay a tatu kwa taratibu.

 Nafasi za nne hadi kumi zimechukuliwa na washiriki kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Somalia, Senegal, Bangladesh, Misri, Niger na Chad.

Mashindano hayo ya kuhifadhi Qur’ani kikamilifu yalifanyika Dubai kuanzia Aprili 14. Kutokana na maambukizi ya corona, ni wakaazi wa UAE tu ndio walishiriki katika mashindano ya mwaka huu.

3966922

captcha