IQNA

18:07 - January 28, 2020
News ID: 3472413
TEHRAN (IQNA) –Maelfu ya wanafunzi wamejisajili katika masomo ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Kwa mujibu wa taarifa, Taasisi ya Makhtoum ya Vituo vya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu imetangaza kuwa jumla ya wanafunzi 3,019 walijisajili katika vituo hivyo mwaka 2019 ambapo asilimia 70 ni wanafunzi wa kike.

Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka jana kulikuwa na warsha 201 za kuhifadhi Qur'ani ambapo kulikuwa na walimu 189 huku 72 miongoni mwao wakiwa ni wanafunzi wa kike.

Warsha hizo za kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika Vituo cha Makhtoum zimefanyika katika maeneo ya Deira, Bur Dubai na Hatta.

Ahmed Muyaha Al Zahed, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Makhtoum ya Vituo vya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu amepongeza kujitokeza idadi kubwa ya wanafunzi wanaotaka kujifadhi Qur'ani Tukufu ambao amesema wamo raia wa UAE na pia raia wa kigeni. Aidha amewapongeza wanafunzi wa kike kwa kuonyesha azma ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Al Zahed amesema lengo la Taasisi ya Makhtoum ya Vituo vya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu ni kuandaa mazingira mazuri ya kuwasaidia wanafunzi kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kufahamu mafundisho ya Kiislamu.

3470464

 

Tags: iqna ، qurani tukufu ، UAE
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: