IQNA

Pakistan yakanusha madai ya kuzungumza na utawala wa Kizayuni

11:09 - December 20, 2020
Habari ID: 3473474
TEHRAN (IQNA) Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan amekanusha kuwepo mashinikizo ya aina yoyote ya kuitaka nchi hiyo ijiunge na safu ya nchi zinazofanya mapatano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Imran Khan ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Pakistan ya Samaa News alipozungumzia tetesi za kuwepo mawasiliano kati ya serikali ya Islamabad na Israel au kufanya safari waziri mmoja wa serikali hiyo kuelekea Tel Aviv na akasisitiza kwamba, huo ni uvumi tu na habari za kubuni zinazotolewa siku hizi na adui ili kuzipotosha fikra za waliowengi.

Kiongozi huyo wa chama tawala cha Pakistan Tehreek-e-Insaf vilevile amesema, ripoti kwamba serikali ya Islamabad inashinikizwa na baadhi ya watawala wa nchi za Kiarabu hususan wa Saudi Arabia iukubali mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni hazina msingi wowote na akasisitiza tena kwamba Pakistan haitautambua utawala huo unaoikalia Quds tukufu kwa mabavu.

Kiongozi huyo wa chama tawala cha Pakistan Tehreek-e-Insaf vilevile amesema, ripoti kwamba serikali ya Islamabad inashinikizwa na baadhi ya watawala wa nchi za Kiarabu hususan wa Saudi Arabia iukubali mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni hazina msingi wowote na akasisitiza tena kwamba Pakistan haitautambua utawala huo unaoikalia Quds tukufu kwa mabavu.

Waziri Mkuu wa Pakistan amesema, wananchi wa Pakistan wako bega kwa bega na wananchi wa Palestina na wanawaunga mkono kikamilifu katika kuhakikisha wanarejeshewa haki zao.

Mara kadhaa, wananchi wa Pakistan wamefanya maandamano makubwa kulaani jinai za utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel za kuwaua wananchi madhulumu wa Palestina na kutangaza uungaji mkono wao wa kudumu kwa malengo matukufu ya Wapalestina na kudhihirisha chuki na ghadhabu zao kwa Wazayuni maghasibu.

Hayo yanajiri wakati ambao mapema mwezi huu wa Disemba, Mfalme wa Morocco Mohammed VI alimwarifu Rais Donald Trump wa Marekani kwenye mazungumzo kwa njia ya simu kuwa amekubali kurejesha mawasiliano ya kiserikali na kuanzisha uhusiano wa kibalozi na utawala wa Israel haraka iwezekanavyo.

Marekani nayo imesema itatambua mamlaka ya Morocco katika eneo la Sahara Magharibi la nchi hiyo ambalo limejitangazia uhuru. Ufalme wa Morocco umetangaza kuwa Marekani hivi karibuni itafungua ubalozi mdogo huko Sahara Magharibi.

Uamuzi huo wa Morocco kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel unafuatia uamuazi sawa na huo uliochukuliwa miezi ya karibuni na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan. Nchi zingine za Kiarabu ambazo zina uhusiano rasmi na utawala bandia wa Israel ni Misri na Jordan.

Hatua ya madola hayo ya Kiarabu kuanzisha uhusiano na Israel inaendelea kulaaniwa kote duniani.

3942131

captcha