IQNA

Indonesia yakanusha kuwa na mpango wa kuanzisha uhusiano na Israel

21:47 - December 24, 2020
Habari ID: 3473487
TEHRAN (IQNA) – Indoneisa imekanusha ripoti kuwa iko tayari kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala bandia wa Israel.

Wizara ya Mambo ya Nje ya indoneisa imetoa taarifa na kupinga kabisa ripoti kuwa ilikuwa inapanga kuwasaliti Wapelestina kwa kuanzisha uhusiano na Israel.

 Teuku Faizasyah, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia amesema hajui taarifa hizo bandia zimetoka wapi na kwamba itafungamana na kuunga mkono uhuru wa Palestina.

Jumuiya ya Maulamaa Indonesia, ambayo ni taasisi ya juu kabisa ya wanazuoni wa Kiislamu nchini humo, imepongeza taarifa ya wizara ya mambo ya nje lakini imeionya serikali kutotumbukia katika mtego wa vishawishi wa kisiasa na kiuchumi kuanzisha uhusiano na Israel.

Hayo yanajiri wakati ambao mkuu wa shirika la kimataifa la ustawi la Marekani ameipendekezea Indonesia rushwa ya dola bilioni 2 ili ikubali kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Adam Buehler amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya Bloomberg na kudai kuwa, kama Indonesia itakukubali pendekezo la rais wa Marekani, Donald Trump la kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, basi Jakarta itapatiwa msaada wa dola bilioni kadhaa na Marekani.

Hadi hivi sasa na kutokana na mashinikizo makubwa ya rais wa Marekani, nchi nne za Kiarabu za Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na Morocco zimetangaza rasmi uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao mikono yake imejaa damu za watu wasio na hatia ndani na nje ya Palestina. Mbali na nchi hizo, Jordan na Misri ni nchi zingine za Kiarabu ambazo zilianzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel miongo kadhaa iliyopita.

Nchi nyingine za Waislamu sasa ziko chini ya mashinikizo makubwa kuwasaliti Wapalestina na kuanzisha uhusiano na utawala dhalimu wa Israel ambao unaendelea kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

3941186

captcha