IQNA

Wanafunzi 80 wa Madrassah ya Qur'ani waliokuwa wametekwa Nigeria wanusuriwa

11:56 - December 21, 2020
Habari ID: 3473476
TEHRAN (IQNA) – Wanafunzi 80 wa Qur'ani Tukufu ambao walikuwa wametekwa kaskazini mashariki mwa Nigeria wamenusuriwa.

Watoto hao wa Madrassah Islamiyya walitekwa nyara Jumamosi na kundi moja la wanamgambo wakati wakirejea kutoka Maulid ya Mtume SAW katika kijiji cha Mahuta, kaskazini magharibi mwa jimbo la Katsina.

Akizungumza na waandishi habari, msemaji wa polisi katika eneo hilo Gambo Isa amesema wanamgambo waliotekeelza utekaji nyara huo pia waliiba ngombe 12.

Amesema baada ya tukio hilo polisi walituma kikosi maalumu kuwanushiri watoto hao na wakafanikiwa katika oparesheni hiyo.

Hayo yanajiri wakati ambao, Ijumaa iliyopita, vyombo vya usalama vya Nigeria vilitangaza habari ya kuachiwa huru karibu wanafunzi wavulana 350 kati ya 520 wa shule ya upili ya eneo la Kankara kaskazini magharibi mwa nchi, waliokuwa wametekwa nyara na kundi la kigaidi la Boko Haram.

Haikubainika wanafunzi hao waliachiwa huru katika mazingira gani, lakini serikali ilisisitiza kuwa haikutoa kikomboleo cha kuachiwa huru watoto hao kwa genge hili la ukufurishaji. Kabla ya tukio hili la Kankara, mwaka 2014 kundi hilo la kigaidi liliwateka nyara pia wanafunzi wa kike 200 huko Chibok Nigeria. 

3473461

captcha