IQNA

Rais Ghani: Waafghani 40,000 wameuawa Afghanistan katika kipindi cha miaka mitano

12:30 - January 10, 2021
Habari ID: 3473543
TEHRAN (IQNA) – Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan amesema vita katika nchi yake vimeua raia zaidi ya 40,000 na katika kipindi hicho ni askari 98 tu wa Marekani waliouawa nchini humo.

“Tokea nichaguliwe kura raia mwaka 2015, idadi ya askari wa Marekani walipoteza maisha Afghanistan ni 98. Hii ni katika hali ambayo sisi, watu wa Afghanistan, tumepoteza zaidi ya raia na wanajeshi 40,000,” Rais Ghani amemuambia Christiane Amanpour wa CNN.

Ghani amemtaka rais mteule wa Marekani Joe Biden kuanisha sera zake kuhusu Afghanistan sambamba na kuwepo mpango wa kuondoa askari wa Marekani walioko Afghanistan.

Marekani iliongoza waitifaki wake katika hujuma ya kijeshi Afghanistan Oktoba 2001 kwa kisingizio cha kukabiliana na ugaidi. Hatahivyo ugaidi umeongezeka nchini humo na hadi sasa usalama haujaweza kupatikana. Uzalishaji wa dawa za kulevya nchini humo umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Katika mwaka 2000 na 2001, ukulima wa mihadarati Afghanistan ulikuwa ni tanu 200 lakini baada ya askari wa Marekani kuvamia nchi hiyo, kiwango hicho kimeongezeka na kufika takribani tani 10,000.

3473654

Kishikizo: afghanistan marekani
captcha