IQNA

Ali al-Houthi: Marekani inaeneza ugaidi duniani

20:11 - January 11, 2021
Habari ID: 3473546
TEHRAN (IQNA)- Muhammad Ali al-Houthi, mjumbe wa Baraza la Kisisa la Harakati ya Wananchi ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, Marekani ndio chimbuko la ugaidi na kwamba, serikali ya sasa ya Donald Trump imekuwa ikitekeleza siasa na sera za kueneza ugaidi dunianii.

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, sera za serikali ya Trump ni ishara ya wazi ya kuweko mgogoro wa kifikra na miamala ya serikali hiyo katu haikubaliki.

Muhammad Ali al-Houthi ambaye pia ni Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Wananchi wa Yemen amesema hayo kufuatia matamshi ya Mike Pompeo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani aliyedai kwamba, amefikia uamuzi wa kuijulisha Kongresi ya nchi hiyo ili iitangaze Harakati ya ansarullah kuwa ni kundi la kigaidi.

Pompeo anatangaza uamuzi huo katika hali ambayo, katika kipindi cha miaka sita iliyopita, muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia umefanya ugaidi na mauaji ya kutisha dhidi ya waanchi wa Yemen sambamba na kuharibu kikamilifu miundombinu mingi ya nchi hiyo masikini ya  Kiarabu.

 

Sehemu kubwa ya silaha zinazotumiwa na muungano huo kuwaulia wananchi wa Yemen na kufanya uharibifu mkubwa zinatoka Marekani, Uingereza na Ufaransa.

Licha ya madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani kuipatia Saudia na washirika wake misaada ya silaha na kipropaganda, lakini utawala wa Aal Saud na waitifaki wake wameshindwa kufikia malengo yao huko Yemen ya kuiingiza madarakani serikali kibaraka kutokana na muqawama na kusimma kidete wananchi wa Yemen. 

3473676

captcha