IQNA

Rais Rouhani alipongeza taifa la Iran kwa kusimama kidete mbele ya ubabe wa Trump

16:20 - January 13, 2021
Habari ID: 3473553
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya amesema kufedheheka na kuaibika utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani katika siku zake za mwisho ni ishara kuwa, ubaguzi wa rangi na ukiukwaji sheria na mambo ambayo hayana mwisho mwema.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo katika kikao cha baraza la mawaziri na kukumbusha kuhusu siku ya kutoroka Iran Shah aliyepinduliwa mnamo Januari 16,1979 kusadifiana na kumalizika utawala wa Trump nchini Marekani na kuongeza kuwa: "Kutoraka Shah ni nembo ya kashfa na kumalizika udikteta na satwa ya mabeberu wa kigeni na leo pia dunia inashuhudiwa tukio lisilo na kifani la kuanguka udiktetea mwingine nchini Marekani."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  amesema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, watu wenye subira wa Iran wamesimama kidete mbele ya utawala wa kigaidi wa Marekani na kuongeza kuwa katika siku hizi hatushuhudii tu kufika ukingoni serikali ya sasa ya Marekani lakini pia tunashuhudia kuanguka sera ya 'mashinikizo ya juu kabisa' dhidi ya taifa kubwa la Iran.

Rouhani amesema: "Katika wakati huu wa mwisho wa miaka mitatu ya vita, utumiaji mabavu na hatua za kigaidi, hali ya kiuchumi ya Iran imekuwa bora  pamoja na kuwepo mashinikizo  mengi na janga la corona."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, sera za mashinikizo ya juu kabisa na ugaidi wa kiuchumi wa Marekani zimefeli kabisa na sasa hata waliotunga sera hizo wanaangushwa.

3947486

Kishikizo: rouhani trump iran marekani
captcha