IQNA

Sayyid Abdulmalik Badruddin al-Houthi

Magaidi wakufurishaji waliibuliwa na Mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi

16:09 - October 20, 2020
Habari ID: 3473278
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi ndiyo ambayo yaliibua makundi ya magaidi wakufirishaji duniani.

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi ndiyo ambayo yaliibua makundi ya magaidi wakufirishaji duniani.

Sayyid Abdulmalik Badruddin al-Houthi amebainisha hayo Jumatatu katika hotuba kwa njia ya televisheni akiwa katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a siku ya Jumatatu na kuongeza kuwa: "Wakufurishaji wanaungwa mkono na Marekani, Ufaransa, nan chi zingine za Magharibi. Wamagharibi wamewaunga mkono Wakufurishaji wakati wanapowaua Waislamu. Marekani na waitifaki wake huko Syria, Yemen na kwingineko wanawaunga mkono wakufurishaji na kuwatumia kuuchafulia Uislamu jina."

Wakufurishaji ni kundi la watu ambao, huwakufurisha Waislamu wote wasiofuata itikadi zao. Aghalabu ya watu hawa ni wafuasi wa itikadi ya Uwahhabi.

Sayyid Abdulmalik Badruddin al-Houthi amebainisha kuwa, upotoshaji na upotokaji ni madhara mawili yaliyozusha mpasuko mkubwa katika safu za Waislamu na kusababisha matatizo makubwa.

Katibu Mkuu wa Ansarullah ameongeza kuwa, maadui wameutumia vibaya kwa maslahi yao upotoshaji unaofanywa ndani ya umma wa Kiislamu kwa ajili ya kuutusi Uislamu na Qur'ani tukufu.

Sayyid Abdulmalik al-Houthi ameeleza kuwa, katika ustaarabu wa Magharibi heshima ya jamii za wanadamu inakanyagwa, uhuru wa watu unahodhiwa, utajiri wao unaporwa na ardhi zao zinavamiwa na kukaliwa kwa mabavu, lakini pamoja na kufanya hayo ustaarabu huo unajinasibu kuwa mtetezi wa haki za binadamu.

Amebainisha pia kwamba, huko Magharibi ni marufuku kuwakosoa Wazayuni na kutilia shaka kwa namna yoyote mauaji ya Wayahudi ya Holocaust, lakini hukohuko Magharibi ni ruhusa mtu kuutusi na kuuvunjia heshima Uislamu na Mitume wa Mwenyezi Mungu.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema, migogoro iliyopo katika nchi za Kiislamu ni matokeo ya umamluki unaofanywa na baadhi kwa ajili ya maadui ya umma na matunda ya hujuma za Mkoloni Magharibi.

3472878

captcha