IQNA

Qarii maarufu wa Qur'ani kutoka Misri, Sheikh Alim Fasada ameaga dunia

7:55 - January 18, 2021
Habari ID: 3473567
TEHRAN (IQNA) – Qarii maarufu wa Misri Sheikh Abdul Alim Fasada ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 73.

Kwa mujibu wa tovuti ya elbalad, Sheikh Fasada alifariki Jumamosi  17 Januari na kuzikwa siku hiyo hiyo.

Sheikh Fasada alikuwa mwanachama wa Jumuiya ya Wasomaji Qur'ani Misri. Alizaliwa mwaka 1947 katika mji wa Billa katika jimbo la Kafr El Shaikh na akawa qarii wa Qur'ani akiwa na umri wa miaka 10.

Aidha aliendeleza masomo yake ya Qur'ani katika Chuo Kikuu cha Al Azhar. Amewahi kushinda katika mashindano mengi ya kitaifa na kimataifa ya kusoma Qur'ani Tukufu. Aidha alikuwa akizitembelea nchi mbali mbali duniani, hasa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kushiriki katika vikao vya kusoma Qur'ani Tukufu.

Sheikh Ahmed Noaina  (Nuaina) , daktari na qarii maarufu wa Misri ametuma salamu za rambi rambi katikaujumbe wake wa Twitter kufuatia kuaga dunia Sheikh Abdul Alim Fasada na kumtaja kuwa mmoja kati ya wasomaji wakongwe zaidi wa Qur'ani Misri. Ameongeza kuwa: "Namuomba Mwenyezi Mungu amrehemu na amjaalie mahala pema peponi na aipe familia yake subira.

 

3948139

captcha