IQNA

Qiraa ya Qur'ani Tukufu ya Qarii wa Misri nchini Bangladesh (+Video)

12:25 - June 15, 2021
Habari ID: 3474007
TEHRAN (IQNA) – Qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Ahmed Ahmed Noaina alitembelea Bangladesh mwaka 2016 ambapo alishiriki katika mahafali kadhaa za Qur'ani.

Klipu hii ni ya qiraa ya Sura Ad Dhuha ya Qur'ani Tukufu katika Msikiti wa Anar Killa huko Chittagong wakati wa Kogamano la 16 la Qiraa ya Qur'ani Tukufu.

Sheikh Noaina  (Nuaina) alizaliwa mwaka 1954 katika mji wa Mutubas nchini Misri na alianza kujifunza Qur’ani Tukufu akiwa na umri wa miaka 4 na kuhifadhi Kitabu hicho Kitukufu akiwa na umri wa miaka minane.

Alijifunza mbinu ya qiraa ya Ustadh Mustafa Ismail huku akiendeleza masomo yake katika taalumu ya daktari wa watoto.

Noaina anatambuliwa kama mmoja kati ya wasomaji bora zaidi wa Qur’ani Misri na ulimwengu mzima katika zama hizi. Sheikh Daktari Nuaina ni qarii mtajika Misri na amepata umashuhuri kutokana na mbinu kumi tafauti anazotumia kusoma Qur'ani Tukufu.

Qarii huyu mashuhuri wa Misri amewahi kusoma katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Misri na nchi nyingi za Kiislamu. Mbali na kuwa msomaji wa Qur'ani pia amehifadhi kikamilifu kitabu hicho kitukufu. Taaluma nyingine ya Sheikh Nuaina ni daktari wa watoto.

3977385

Kishikizo: Noaina ، qiraa
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha