IQNA

Qarii Noaina wa Misri asoma Qur'ani akiwa amevaa barakoa + Video

12:37 - January 23, 2021
Habari ID: 3473584
TEHRAN (IQNA) – Klipu ya video imesambaa katika mitandao ya kijamii ikimuoneysha qarii maarufu wa Misri, Sheikh Ahmed Ahmed Noaina akisoma Qur'ani Tukufu akiwa amevalia barakoa.

Katika klipu hiyo, Sheikh Noaina anasoma aya ya 73 ya Sura az-Zumar isemayo: "  Na walio mcha Mola wao Mlezi wataongozwa kuendea Peponi kwa makundi, mpaka watakapo fikilia, nayo milango yake imekwisha funguliwa. Walinzi wake watawaambia: Salaam Alaikum, Amani iwe juu yenu! Mmet'ahirika. Basi ingieni humu mkae milele."

Sheikh Noaina  (Nuaina) alizaliwa mwaka 1954 katika mji wa Mutubas nchini Misri na alianza kujifunza Qur’ani Tukufu akiwa na umri wa miaka 4 na kuhifadhi Kitabu hicho Kitukufu akiwa na umri wa miaka minane.

Alijifunza mbinu ya qiraa ya Ustadh Mustafa Ismail huku akiendeleza masomo yake katika taalumu ya daktari wa watoto.

Noaina anatambuliwa kama mmoja kati ya wasomaji bora zaidi wa Qur’ani Misri na ulimwengu mzima katika zama hizi. Sheikh Daktari Nuaina ni qarii mtajika Misri na amepata umashuhuri kutokana na mbinu kumi tafauti anazotumia kusoma Qur'ani Tukufu.

Qarii huyu mashuhuri wa Misri amewahi kusoma katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Misri na nchi nyingi za Kiislamu. Mbali na kuwa msomaji wa Qur'ani pia amehifadhi kikamilifu kitabu hicho kitukufu. Taaluma nyingine ya Sheikh Nuaina ni daktari wa watoto.

3949252

 

captcha