IQNA

15:05 - February 13, 2021
Habari ID: 3473647
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuyaelewa mafundisho sahihi ya Qurani Tukufu ndio ufunguo wa kuongoka katika njia iliyonyooka tabaka la vijana.

Rais Rouhani amesema hayo leo Jumamosi katika Ofisi ya Rais mjini Tehran wakati wa  hafla ya kuwaenzi wahudumu wa Qurani Tukufu na kuongeza kuwa, kizazi cha vijana kitaongoka iwapo kitafuata vizuri na kuyaelewa mafundisho sahihi na miongozo ya kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu.

Kadhalika Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekumbusha kuwa, "Rajab na Shaaban ni miezi miwili inayotuandaa kuupokea mwezi mtukufu wa baraka wa Ramadhani." Leo Jumamosi imesadifiana na tarehe Mosi Rajab, mwezi uliojaa rehema na fadhila tele. 

Amebainisha kuwa, "Allah hutupa uongofu katika miezi ya Rajab na Shaaban ili tuweze kujiandaa kwa saum (funga) na qiyam (visimamo vya ibada)."

Dakta Rouhani ameendelea kuuasa Umma wa Kiislamu kwa kuuambia kuwa, waumini wa Kiislamu wanapaswa kuzidhibiti ndimi zao na kuchunga matamshi yao. Pia wanapaswa kuisoma Qurani Tukufu kwa sauti nzuri kwani kufanya hivyo ni sawa na kutumia lugha kwa ufasaha.

 

 

3953727

 

Kishikizo: iran ، qurani tukufu ، hassan rouhani ، vijana
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: