IQNA

21:39 - January 23, 2021
News ID: 3473585
TEHRAN (IQNA) – Wapalestina wameandaman katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kupinga hatua ya utawala haramu wa Israel kuendelea kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.

Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel walishambulia waandamanaji hao katika mji wa Beit Dajan, mashariki mwa mji wa Nablus.

Wapalestina waliandamana katika eneo la Kafr Qaddum, mashariki mwa mji wa Qalqilya ambapo walishambuliwa na wanajeshi wa Israel.

Katika kipindi cha wiki za hivi karibuni, na kwa kutumia fursa ya siku za mwishoni mwa utawala wa Donald Trump huko Marekani, Wazayuni walizidisha jinai zao dhidi ya Wapalestina, kuvunja nyumba zao, kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kuwateka nyara vijana wa taifa madhlumu la Palestina katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Utawala wa Kizayuni wa Israel una nia ya kujenga zaidi ya nyumba laki 4 nyingine katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, ikiwa ni muendelezo wa kupora ardhi za wananchi wanaodhulumiwa kila upande wa taifa la Palestina.

Utawala wa Kizayuni wa Israel, ambao unapata himaya kamili ya Marekani, umekiuka azimio 2334 la Baraza la Usalama, ambalo Disemba 2016 lilitaka usitishwaji wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. 

Karibu jamii nzima ya kimataifa inasisitiza kuwa hatua ya Israel kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi ni kinyume cha sheria.

3473766

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: