Hujuma hizo kwa kawaida hufanyika kwa himaya ya jeshi la utawala haramu wa Israel.
Wizara ya Wakfu ya Palestina imetoa taarifa Jumatano ikisema: "Mwezi Desemba kulikuwa na ongezeko la hujuma ya vikosi vya utawala ghasibu wa Israel na walowezi wa Kizayuni dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa."
Taarifa hiyo imesema: "Uvamizi huu unalenga kuunda hali mpya katika msikiti kwa kuruhusu wavamizi kufanya ibada za kidini za Kiyahudi."
Askari wa utawala wa Israel, wizara ilisema, wanatoa ulinzi kwa wavamizi, wanazuia kazi za walinzi wa msikiti na kuwazuia waumini wa Kiislamu kuingia msikitini hapo.
Jumapili, waziri wa mawasiliano wa Israel Shlomo Karhi, akiwa ameandamana na walowezi wa Kizayuni walivamia na kuingia kwa lazima katika uwanja wa msikiti huo na kufanya ibada ya Kiyahudi katika eneo la chini ya Ukuta wa Magharibi (Ukuta wa Al-Buraq).
Wiki iliyopita, waziri wa usalama wa kitaifa wa mrengo wa kulia wa Israel Itamar Ben-Gvir alivamia msikiti huo kuadhimisha sikukuu ya Kiyahudi chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Msikiti wa Al-Aqsa ni eneo la tatu takatifu zaidi kwa Waislamu duniani. Wayahudi wanaita eneo hilo kuwa eti ni 'Mlima wa Hekalu', wakisema lilikuwa eneo la mahekalu mawili ya Kiyahudi katika nyakati za kale.
Utawala haramu wa Isarel ulikalia kwa mabavu al-Quds Mashariki, ambako Al-Aqsa iko, wakati wa Vita vya Waarabu na Israeli vya 1967. Baadaye Israel iliteka jiji lote mwaka 1980 katika hatua ambayo haijawahi kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa.
3491300