IQNA

17:58 - March 01, 2021
News ID: 3473691
TEHRAN (IQNA) – Mwaka 1994, qarii mashuhuri wa Misri marhum Sheikh Abolainain Shoaisha alitembelea Iran ambapo alishiriki katika kikao cha qiraa ya Qur'ani Tukufu katika Haram ya Hadhrat Abdul Adhim Hassani AS mjini Tehran.

Akiwa hapo alisoma aya kadhaa za Surah an-Nisaa katika kikao ambacho pia kilihudhuriwa na maqarii wengine maarufu wa Misri, Sheikh Shahat Anwar na Sheikh Ahmed Raziqi.

Sheikh Shoaisha alizaliwa Kafarsheikh kaskazini mwa Misri mwaka 1343 Hijri (1922). Alianza kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu akiwa mtoto mdogo. Shoaisha alipata umashuhuri kama karii kuanzia mwaka 1936 alipokuwa akihudhuria darsa za kiraa ya Qur'ani mjini Mansura. Alianza kusoma Qur'ani katika Radio ya Misri mwaka 1939. Shoaisha aliathiriwa sana Ustadh Sheikh Muhammad Raf'at, karii mashuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu. Awali alifuata mbinu ya usomaji wa Raf'at lakini baadaye aliibua mbinu yake ya kipekee ya qiraa.
Ustadh Shoaisha alitembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mara kadhaa kama jaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.

Sheikh Abulainain Shoaisha aliiaga dunia Juni 23, 2011 akiwa na umri wa miaka 89.

 

3956677

Tags: iran ، Shoaisha ، qiraa ، qurani tukufu
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: