IQNA

Kiongozi wa Hizbullah amshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa ujumbe wake

19:17 - March 06, 2021
Habari ID: 3473709
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amemtumia ujumbe Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei akimshukuru kwa kuwa kwake muda wote na wananchi wa Lebanon na kwa hatua yake ya kutoa mkono wa pole kufuatia kufariki dunia Sheikh Ahmad al Zin, mwanachuoni mkubwa wa wa Kisuni wa Lebanon.

Televisheni ya al Mayadeen imetangaza habari hiyo leo na kuongeza kuwa, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amemtumia ujumbe Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei akimuhakikishia kuwa ataendeleza njia ya marhum Sheikh Ahmad al Zein na malengo matukufu ya Hizbullah ya Lebanon.

Wiki iliyopita, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alimtumia ujumbe Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon akimpa mkono wa pole kufuatia kifo cha mwanachuoni mkubwa na mwanaharakati, Sheikh Ahmad al Zein

Sheikh Ahmad al Zein alikuwa mmoja wa maulamaa wakubwa wa Kisuni nchini Lebanon. Alikuwa kadhi wa mji wa Saida (Sidon) na Mkuu wa Jumuiya ya Maulamaa Waislamu nchini Lebanon. Mwanachuoni huyo mkubwa wa Kisuni wa Lebanon, alifariki dunia wiki iliyopita. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Kiislamu alitoa mkono wa pole kwa taifa zima la Lebanon na Waislamu kiujumla kwa kumpoteza mwanachuoni huyo mkubwa.

Sheikh Ahmad al Zein alikuwa mwanaharakati mkubwa wa kupigania ukombozi wa Palestina na kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo hili. Alikuwa anaamini kuwa, muqawama ndiyo njia pekee ya kuweza kuikomboa Quds na Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa. Alikumbana na matatizo mengi kutoka kwa Wazayuni katika mapambano yake hayo kama vile majaribio ya kumuua kigaidi, kumuudhi na kumuwekea vizingiti katika harakati zake.

/3957789

captcha