Katika ujumbe wake huo, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesisitiza kuwa, nguvu za kiimani zimewafungulia wanawake wa Iran njia ya kufanya jihadi kubwa na kuwapa fursa ya kuingia na kufanya maajabu ya kipekee katika medani zinazohitaji ushujaa, kujitolea na ubunifu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kisilamu ametoa mifano akisema: Kuanzia medani za elimu, utafiti na teknolojia hadi katika nyuga za fasihi na sanaa; mpaka kwenye kudhihirisha vipaji na kung'ara katika chanjaa za kijamii, kisiasa na uongozi na hatimaye kwenye uwanja wa kujitolea kwenye medani za afya na kuhudumia wagonjwa katika mazingira hatari sana na magumu, na muhimuu kuliko yote ustawi kimaanawi mwanamke wa Kiirani, fakhari zote hizo zinashuhudiwa kutokana na baraka za Jamhuri ya Kiislamu na mafundisho matukufu ya dini ya Kiislamu.
Ayatullah Khamenei pia amesisitiza kuwa, mwanamke wwa Iran leo hii amefanikiwa kujikurubisha kwenye maadili mazuri ya heshima na usafi unaotakiwa na Uislamu licha ya mashambulizi makubwa ya utamaduni fasidi wa Magharibi ambao umeporomoka vibaya kimaadili na ambao uliwaathiri mno wanawake wa Iran wakati wa utawala wa Kipahlavi humu nchini. Lakini leo hii, ni fakhari kubwa kuona mwanamke wa Iran amejikurubisha kwenye maadili mazuri na safi yanayotakiwa na dini tukufu ya Kiislamu.