IQNA

15:06 - March 10, 2021
News ID: 3473722
TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamemkamata Khatibu wa Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem).

Kwa mujibu wa Televisheni ya Al Jazeera, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel leo Jumatano walishambulia nyumba ya  Sheikh Ekrima Sa'id Sabri, Khatibu wa Msikiti wa Al Aqsa na mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu Quds.

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni hawakutoa sababu yoyote ya kumkamata mwanazuoni huyo nyumbani kwake katika mtaa wa Al-Sawana mjini Quds. Aidha haijulikani Sheikh Sabri amepelekwa wapi baada ya kukamatwa na wanajeshi hao wa Israel.

Sheikh Sabri amewahi kukamatwa mara kadhaa na wanajeshi wa Israel kwa visingizio mbali mbali kama vile kuunga mkono mapambano ya ukombozi wa Palestina na kupinga wazi hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel. Aidha Sheikh Sabri ni mpinzani mkali wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi.

Utawala wa Kizayuni unatekeleza misingi mitatu mikuu ambayo ni kuugawa utumiaji wa Msikiti wa Al Aqsa kisehemu na kiwakati, kuchimba mashimo ya chini kwa chini na kandokando ya msikiti na kuyahudisha maeneo ya jirani na mahala hapo patakatifu.

Hii ni katika hali ambayo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limethibitisha tena kwamba msikiti mtukufu wa Al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu ni milki ya Wapalestina.

3958822

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: