IQNA

Hamas yalaani hatua ya Wazayuni kufanya ibada zao ndani ya Msikiti wa Al Aqsa

21:47 - October 07, 2021
Habari ID: 3474394
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani hatua ya mahakama moja ya utawala bandia wa Israel kuwaruhusu walowezi wa Kizayuni kuingia katika uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa kwa ajili ya kufanya ibada zao.

Msemaji wa Hamas amesema uamuzi huo ni hujuma ya wazi dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Hamas imesema hatua hiyo ni katika njama za kuugawa kiwakati na kimahali Msikiti mtukufu wa Al-Aqsa wenye lengo la kuuyahudisha msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Utawala wa Kizayuni ambao unaungwa mkono kikamilifu na Marekani katika hatua zake hizo haramu umedhamiria kubadilisha muundo wa kijiografia na kidemografia wa maeneo ya Palestina; ili kwa kuyazayunisha au kuyahudisha maeneo hayo na kuhakikisha unazihodhi na kuzidhibiti kikamilifu ardhi za Wapalestina.

3475927/

captcha