IQNA

SheikhAdam Ahmad Tsoho

Serikali ya Nigeria haitaki kumuachilia huru Sheikh Zakzaky

18:36 - March 30, 2021
Habari ID: 3473772
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Nigeria inaogopa misimamo na fikra za Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini humo na hivyo haina nia ya kumuachilia huru.

Akizungumza na gazeti la Islam Times, Sheikh Adam Ahmad Tsoho , mwakilishi wa Sheikh Zakzaky katika mji wa Jos nchini Nigeria amesema kile ambacho kimepelekea serikali ya Nigeria iwe na hofu sana ni kuwa Sheikh Zakzaky hatenganishi siasa na dini katika misimamo yake.

Amesema hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky na mke wake gerezani ni mbaya na wamenyimwa ruhusa ya kuenda hospitalini kupata matibabu.

Aidha amesema  pamoja na kuwa Sheikh Zakzaky ni Muislamu wa madhehebu ya Shia lakini anapendwa na Waislamu wa madhehebu ya Sunni na pia Wakristo kutokana na msimamo wake wa kutetea haki na uadilifu na pia azma yake wa kuunga mkono wa umoja wa watu wote wa Nigeria ambao wanadhulumiwa na serikali na madola ya kibeberu.

Sheikh Ibrahim Zakzaky

Halikadhalika Sheikh Adam Ahmad Tsoho serikali ya Nigeria inawashinikiza Waislamu wa madhehebu ya Shia kwa sababu inaamurishwa kufanya hivyo na Saudi Arabia, kupitia taasisi za Kiwahhabi nchini humo. Aidha amesema mbali na Saudia, utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani pia zinahusika katika kuihimiza serikali ya Nigeria iwakandamize Waislamu wa kishia nchini Nigeria.

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake walikamatwa na vyombo vya dola vya Nigeria tarehe 13 Disemba mwaka 2015 katika shambulizi lililofanywa na askari wa nchi hiyo dhidi ya kituo cha kidini cha Baqiyyatullah katika mji wa Zaria. 

Karibu wafuasi 1,000 wa harakati ya Kiislamu ya Nigeria waliuawa kwa umati na vikosi vya usalama katika shambulizi hilo.

3961784

captcha