IQNA

Waislamu Nigeria

Serikali ya Nigeria yatakiwa kuunga mkono mafunzo ya Qur'ani Tukufu

13:56 - December 11, 2023
Habari ID: 3478019
IQNA - Mhubiri mkuu wa Kiislamu katika Jimbo la Oyo, kusini magharibi mwa Nigeria, alisisitiza haja ya serikali kuunga mkono masomo ya Qur'ani Tukufu na Kiislamu nchini humo.

Ali Abdulssalam, anayefundisha katika Taasisi ya Kuhifadhi Qur'ani ya Ali, (AIQM) Ibadan, aliitaka serikali kuzingatia kuingiza Quran na Kiarabu katika mitaala ya shule za msingi na sekondari.

Alisema hilo litawajengea watoto mafunzo ya Uislamu katika umri mdogo, ili kuwafanya kuwa raia wenye manufaa.

Akizungumza katika Ibadan katika Mahafali ya Nne ya Haflah ya kuhifadhi kikamilifu Qur'ani Tukufu, Ali alisema kwa kuzingatia mchango wa Uislamu katika uadilifu wa jamii, serikali inapaswa kutambua na kuunga mkono Qur'ani na Mafunzo ya Kiislamu.

Alisema Uislamu unafanya utumishi mkubwa kwa nchi kwa kuhakikisha vijana wanapata lishe bora ya kiroho inayotakiwa, hivyo kupunguza uhalifu katika jamii.

“Tunachukua fursa hii pia kusisitiza haja ya serikali kutengeneza ajira kwa wahitimu wa shule za Kiarabu na Quran nchini. Hili pia litasafisha jamii, kwani vijana wengi wanaomcha Mungu wataajiriwa, jambo ambalo litapunguza uhalifu katika jamii.

“Waislamu ndio wakombozi wa dunia. Mwenyezi Mungu ametupa jukumu la kimsingi la kuamrisha wema na kukataza maovu. Tumejitwika jukumu la kuwafundisha vijana wa Kiislamu kuhifadhi Quran, maadili ya Kiislamu na adabu.

"Kuhifadhi Qur'an Tukufu kamwe hakuwezi kuzuia maendeleo ya mtoto, bali kutaboresha zaidi kwa sababu imekuwa dhahiri kwamba kuwapa watoto elimu ya Magharibi tu bila elimu ya Qur'ani ni kama gari zuri lenye injini mbovu.

3486368

Kishikizo: qurani tukufu nigeria
captcha