IQNA

18:35 - April 17, 2021
News ID: 3473822
TEHRAN (IQNA) – Maandamano yamefanyika katika mji mkuu wa Nigeria, ya kutaka kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini humo, Sheikh Ibrahim Zakzaky aachiliwe huru.

Kwa mujibu wa taarifa mamia ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky walishiriki katika maandamano yaliyofanyika katika mtaa wa Garki.

Waandamanaji wamelalamikia vikali kuendelea kushikiliwa Sheikh Zakzaky na mke wake na kutaka waachiliwe huru mara moja na bila masharti.

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake walikamatwa na vyombo vya dola vya Nigeria tarehe 13 Disemba mwaka 2015 katika shambulizi lililofanywa na askari wa nchi hiyo dhidi ya kituo cha kidini cha Baqiyyatullah katika mji wa Zaria. 

Karibu wafuasi 1,000 wa harakati ya Kiislamu ya Nigeria waliuawa kwa umati na vikosi vya usalama katika shambulizi hilo.

Mwaka 2016, Mahakama ya Kifiderali iliamuru Sheikh Zakzaky aachiliwe huru lakini serikali imekaidi amri hiyo.

تظاهرات شیعیان نیجریه در اعتراض به ادامه حبس غیرقانونی شیخ زکزاکی

تظاهرات شیعیان نیجریه در اعتراض به ادامه حبس غیرقانونی شیخ زکزاکی

تظاهرات شیعیان نیجریه در اعتراض به ادامه حبس غیرقانونی شیخ زکزاکی

تظاهرات شیعیان نیجریه در اعتراض به ادامه حبس غیرقانونی شیخ زکزاکی

3474467

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: