IQNA

18:28 - April 18, 2021
News ID: 3473828
TEHRAN (IQNA)- Duru ya Tisa ya Mashindano ya Qur’ani kwa ajili ya walemavu imeanza Jumamosi mjini Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Kwa mujibu wa taarifa, mashindano ya mwaka huu yana washiriki 330 ambao wanashiriki kwa njia ya intaneti kutokana na maambukizi ya COVID-19.

Washiriki wanashindana katika kategoria mbali mbali za kuhifadhi Qur’ani na yataendelea kwa muda wiki mbili.

Lengo la mashindano hayo limetajwa kuwa ni kuwahimiza wenye ulemavu kuhifadhi Qur’ani Tukufu na pia kubaini vipaji miongoni mwao.

3965362

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: