IQNA

16:47 - September 28, 2019
News ID: 3472152
TEHRAN (IQNA) – Mashindano yajayo ya kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yamepangwa kufanyika katika Mji Mtakatifu wa Mashhad, kaskazini mashariki mwa nchi.

Hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam Seyyid Mehdi Khamoushi, mkuu wa Shirika la Wakfu la Iran wakati akifungua Mashindano ya 42 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Akizungumza Jumamosi katika mji wa Isfahan, kati mwa Iran, amesema washindi katika mashindano hayo ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu,  wataiwakilisha Iran katika mashindano ya kimataifa yatakayofanyika Mashhad. Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu hufanyika kila mwaka nchini Iran. Mwaka huu  Mashindano ya 36 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yalifanyika mjini Tehran.

Mbali na mashindano ya kawaida ya wanaume, mwaka huu pia kulifanyika mashindano maalumu kwa ajili ya wanawake, wanafunzi wa vyuo vya kidini, wanafunzi wa shule na walemavu wa macho ambao watashindana katika kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.  Washiriki wa mashindano hayo ya Qur'ani walishindana katika kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu.

Mwaka huu washiriki 184 wa mashindano ya Qur'ani kutoka nchi 84 walifanikiwa kufika katika nusu fainali ya mashindano.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano ya kimatiafa ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani ya Iran kila mwaka ambapo huwa na washiriki kutoka kila kona ya dunia.

/3845424

 

Name:
Email:
* Comment: