IQNA

Khalid Meshaal: Hamas itahakikisha Israel inaachilia huru wafungwa Wapalestina

18:04 - April 19, 2021
Habari ID: 3473830
TEHRAN (IQNA)- Kadhia ya wafungwa Wapalestina wanaoshikiliwa katika magereza ya utawala wa Kizayuni wa Israel ni kipaumbele kwa watu wa Palestina.

Hayo yamesemwa na Khalid Meshaal, kiongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas)  ambaye amesisitiza kuwa, harakati hiyo ina azma ya kuhakikisha Wapalestina wanaoshikliwa mateka na Israel wanaachiliwa huru.

"Tunatangaza kuwa tuna azma ya kufikisha ujumbe wa wafungwa katika majukwaa yote ya kitaifa na kimataifa," amesema Meshaal katika mahojiano kwa Mnasaba wa Siku ya Wafungwa Wapalestina Jumapili.

Ameongeza kuwa adui Mzayuni atalazimika kuwaachiwa huru mateka hao kwa lugha tu ya muqawama na si kupitia mazungumzo na majadiliano. Khalid Mash'al amesisitiza kuwa: sisi hatimaye tutamlazimisha adui Mzayuni kuwaachia wafungwa wa Kipalestina. 

Meshaal ameashiria namna jukumu kuu la Hamas na makundi mengine ya muqawama ya Palestina kuwa ni kuhakikisha kuwa mateka wanaachiwa huru kutoka katika jela za adui na kutaka kushadidishwa muqawama katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan kwa lengo la kukabiliana na uvamizi na jinai za adui Mzayuni. Amesema kuwa, ni kupitia muqawama pekee ndipo ardhi na mateka wa Kipalestina watakapokuwa huru. 

/3474487

captcha