IQNA

22:05 - April 20, 2021
News ID: 3473835
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufalme wa Saudi Arabia Jumatatu imechapisha picha za walinzi wanawake wakiwa katika Msitiki Mtakatifu wa Makka, al-Masjid al-Ḥaram.

 

Hii ni mara ya kwanza kwa wanawake kupewa jukumu la kulinda usalama katika msikiti huo mtakatifu zaidi katika Uislamu.

Picha zilizosambazwa mitandaoni zinawaonyesha walinzi wanawake wakiwa wamevalia sare zao waijishughulisha majukumu yao ya kiusalama huku waumini wanaotekeleza umrah au wanaosali wakiwa wanaendelea na ibada. Walinzi hao wameonokana wakiwa wamevalia barakoa ikiwa ni katika hatua ambazo zinachukulia kuzia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Hatua ya kuanza kazi walinzi hao wanawake katika Msikiti Mtakatifu wa Makka imekabiliwa na hisia mseto huku baadhi wakikosoa hatua hiyo na baadhi wakiunga mkono na kusema walenzi hao wataweza kuwasaidia wanawake wanaofika msikitini hapo.

Women Security Guards on Duty for at Masjid Al-Haram   

3474511

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: