Idara ya Uratibu wa Darasa na Vikao vya Qur’ani katika Msikiti Mkuu imetangaza uzinduzi wa kozi hiyo.
Kozi hii ya Qur’ani inajumuisha sehemu tatu muhimu: kuhifadhi, kupitia aya, na usomaji. Vipindi hivyo vinaendeshwa kwa mujibu wa mipango ya kielimu ya Qur’ani inayofanyika ndani ya Msikiti Mkuu wa Makka.
Kitengo cha wanawake cha idara hiyo kinasimamia utekelezaji wa kozi hii ya Qur’ani, na kupanga programu zake za kielimu na kiutendaji.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, jumla ya vikao 60 vya Qur’ani vimepangwa kwa kozi ya kiangazi ya wanawake, na zaidi ya wanafunzi 1,500 wa Qur’ani wameshiriki na kufaidika na vipindi hivyo.
Walimu na wasomi wa kike waliobobea katika usomaji na uhifadhi wa Qur’ani ndiyo wanaotoa mafunzo katika kozi hii.
Kozi hii ni miongoni mwa shughuli zinazolenga kuimarisha athari za vipindi vya elimu ya Kiislamu, kueneza ujumbe wa Qur’ani na kuwafundisha mahujaji wa kike kutoka makundi mbalimbali, kwa mujibu wa waandaaji.
3493897