IQNA

Misikiti kadhaa India yatumiwa kama wodi wakati huu wa janga la COVID-19

21:31 - April 28, 2021
Habari ID: 3473858
TEHRAN (IQNA)- Huku India ikiendelea kusakamwa na ongozeko kubwa sana la maambukizi ya COVID-19, hospitali na vituo vya afya nchini humo ambazo hazina nafasi tena sasa zinapokea msaada wa Waislamu nchini humo.

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa idadi ya waliofariki kutokana na virusi vya corona nchini India imepindukia watu laki mbili leo.

 Hii ni baada ya zaidi ya watu elfu tatu wengine kufariki katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita hiyo ikiwa ni rekodi ya vifo kwa siku moja. Kwa sasa India imesajili visa milioni 18 vya maambukizi na katika masaa ishirini na nne yaliyopita watu 360,000 wameambukizwa virusi vya corona.

Mwezi huu wa Aprili pekee, nchi hiyo imeshuhudia maambukizi milioni sita. Mlipuko huo wa maambukizi ambao unadaiwa kutokana na aina mpya ya kirusi pamoja na mikutano mikubwa kisiasa na kidini, imesababisha hospitali kulemewa na ukosefu wa vitanda, dawa na gesi muhimu ya oksijeni. India kufikia sasa imewachoma chanjo watu milioni 150 na kuanzia Jumapili, mtu yeyote aliye na umri wa miaka 18 au zaidi ataruhusiwa kupokea chanjo.

Kutokana na hali hiyo mbaya ya maambukizi Waislamu India wanatoa misaada kukabiliana na hali hiyo. Kwa mfano Msikiti wa Jahangirpura mjini Vadodara katika jimbo la Gujarat sasa umegeuzwa na kuwa hospitali yenye uwezo wa vitanda 50. Aidha msikiti wa Darool Uloom mjini humo umefungua milango yake kwa wagonjwa wa corona na sasa una vitanda 142 vyenye mashine za oxigeni.  Mwanachama wa kamati ya msikiti huo Ashfaq Malek Tandalja amesema msikiti huo una uwezo wa kubeba vitanda 1,000 lakini tatizo ni kuwa hakuna oxijeni ya kutosha.

Naye Pyare Khan, tajiri mkubwa katika mji wa Nagpur katika jimbo la Maharashtra ametoa msaada wa tani 400 za okijeni kwa hospitali mjini humo.

Shirika la Afya Duniani limesema litatuma misaada ya dharura kuisaidia India kukabiliana na wimbi kubwa la maambukizi ya corona.

3474577

Kishikizo: india waislamu Corona
captcha