IQNA

Iran yalaani hujuma ya Wazayuni dhidi ya Wapalestina ndani ya Msikiti wa Al Aqsa

12:21 - May 08, 2021
Habari ID: 3473887
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali hujuma ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa wakati Wapalestina walipokuwa katika eneo hilo takatifu.

Katika taarifa mapema leo, Saeed Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema:  “Iran inalaani hujuma ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni unaokalia Quds kwa mabavu dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu  ambapo Wapalestina kadhaa waliokuwa wamefika hapo wameuawa shahidi au kujeruhiwa katika Ijumaa ya Mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Siku ya Kimataifa ya Quds.”

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: “Jinai hii ya kivita kwa mara nyingine inaweka wazi utambulisho wa kijinai wa utawala haramu wa Kizayuni na hivyo kuna udharura kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka za kusitisha ukiukwaji wa misingi ya ya haki za binadamu.”

Khatibzadeh aidha amesema: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mbali na kulaani jinai hiyo ya wazi dhidi ya binadamu inatuma salamu za rambi rambi kwa familia za waliouawa shahidi katika tukio hilo na inataka Umoja wa Mataifa na taasisi zingine za kimataifa zitekeleza wadhifa wao na kukabiliana na jinai hii ya kivita.”

جنایات صهیونیستها در روز قدس در مسجدالاقصی؛ ۲ شهید و ۲۰۵ زخمیMsemaji wa Wizara ya Mambo ya Iran ameendelea kusema kuwa  Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina fakhari kuwa inasimama pamoja na watu wa Palestina na inatoa wito kwa nchi zote duniani hasa nchi za Kiislamu kutekeleza majukumu yao ya kihistoria na kuwa pamoja na watu wa Palestina katika kukabiliana na Wazayuni wavamizi.

Duru za habari zinasema kuwa, Ijumaa usiku wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliwashambulia Wapalestinsa waliokuwa wakiswali katika Msikiti wa Al Aqsa. Taarifa zinasema wanajeshi hao wa Kizayuni walifunga milango ya Msikiti wa Al Aqsa na kuwahujumu Wapalestina waliokuwa wakiswali.

 Katika hujuma hiyo ya kinyama Wapalestina wasiopungua 53 walijeruhiwa wakati wanajeshi wa Kizayuni walipoingia ndani ya Msikiti wa Al Aqsa.

3474648

Kishikizo: AQSA ، QUDS ، PALESTINA ، israel ، khatibzadeh
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :