IQNA

Jinai za Israel

Mwanasoka Mfaransa Pogba atangaza mshikamano na watoto Wapalestina waliouawa na Israel

19:38 - August 14, 2022
Habari ID: 3475621
TEHRAN (IQNA) – Mcheza soka mashuhuri wa Ufaransa Paul Pogba ameonyesha mshikamano na Wapalestina katika Ukanda wa Gaza baada ya mashambulio ya hivi karibuni ya anga ya jeshi la utawala katili wa Israel kwenye eneo hilo na kuua shahidi Wapalestina zaidi ya 45 wakiwemo watoto 19.

Mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye pia ni nyota wa klabu ya Juventus ya Italia alitumia akaunti yake ya Instagram na kuweka picha za watoto waliopoteza maisha wakati wa mashambulizi ya hivi punde ya Israel huko Gaza.

Kiungo wa kati wa soka aliandika hivi, "Mwenyezi Mungu awalinde watu wa Gaza."

Mara tu alipoweka picha hiyo kwenye ukurasa waka wa Instagram, ilisambaa kwa kasi huku watu wakisambaza picha hizo zaidi.

Mtumiaji wa Twitter aliandika, "Mchezaji kandanda Muislamu wa Ufaransa, mchezaji wa Juventus Paul Pogba anaunga mkono dhamira ya Palestina kwa mara nyingine tena kwa kuchapisha picha za watoto waliouawa wakati wa uvamizi wa Israel huko Gaza."

Mwingine alisema, "Mchezaji Muislamu wa Ufaransa wa Juventus Paul Pogba anarejesha uungaji mkono wake kwa watu wa Palestina kwa kuweka picha za watoto wa Gaza waliouawa wakati wa uvamizi wa 2022, akitoa maoni 'Mungu awaokoe watu wa Gaza.

Ndege za kivita za Israel zilifanya mashambulizi ya anga katika Ukanda wa Gaza wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, Wapalestina wasiopungua 45, wakiwemo wanawake na watoto, waliuawa katika mashambulizi hayo ya anga, huku wengine 360 ​​wakijeruhiwa.

/3480078

captcha