IQNA

Pogba aondoa pombe mezani katika kikao na wanahabari baada ya mechi

12:45 - June 17, 2021
Habari ID: 3474013
TEHRAN (IQNA)- Paul Pogba mchezaji mashuhuri wa Timu ya Taifa ya Ufaransa ameondoa chupa ya pombe iliyokuwa imewekwa mbele yake kwa lengo la kutangaza shirika moja la utegenezaji pombe.

Pogba ambaye pia ni mchezaji wa Klabu ya Manchester United anafahamika kuwa Mwislamu mwenye kufungamana na mafundisho ya dini na hivyo hakutaka kufungamanishwa na utangazaji pombe.

Pogba alichukua hatua hiyo wakati alipokuwa akihutubia kikao na waandishi habari Jumatatu baada ya mechi ya Euro 2020 ambapo Ufaransa iliinyuka Ujerumani moja sifuri.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alionekana kukasirika wakati alipogundua mbele yake kulikuwa na chupa ya pombe ya shirika moja kubwa na papop hapo akaichukua chupa hiyo na kuiweka chini isweze kuonekana wakati akizungumza na waandishi habari.

Hivi karibuni pia mchezaji wa Ureno Christiano Ronaldo aliiondoa chupa ya Coca-Cola iliyokuwa mbele yake wakati wakati akizungumza na waandishi habari baada ya mechi. Alisema anafadhilisha kunywa maji badala ya Coca Cola.  

3474966

Kishikizo: pogba ، mechi ، pombe
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :