IQNA

Mauaji ya Mashia Afghanistan yatambuliwe kuwa mauaji ya kimbari

18:37 - May 19, 2021
Habari ID: 3473927
TEHRAN (IQNA)- Wanaharakati wa haki za binadmau na utamaduni nchini Afghanistan wameutaka Umoja wa Mataifa utambue rasmi mauaji ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Afghanistan katika miaka ya hivi karibuni kuwa ni mauaji ya kimbari.

Ingawa watu wa Afghanistan kwa ujumla wanakabiliwa na vita na ukosefu wa usalama, lakini ongezeko la mauaji ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo kumeplekea kadhia yao iangaziwe na watetezi wa haki. Wanaharakati wengi wanaamini kuwa, mauaji dhidi ya Mashia, hasa magharibi mwa mji mkuu Kabul, ni dalili tosha kuwa kuna kampeni maalumu ya mauaji ya Mashia nchini Afghanistan.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi hujuma kadhaa za kigaidi zimelenga misikiti, vituo vya elimu, shule, viwanja vya michezo na hospitali katika maeneo yenye Mashia wengi mjini Kabul.

Hujuma hizo za hivi karibuni zimepelekea mamia ya raia wasio na hatia kuuawa na aghalabu ya wanaopoteza maisha ni vijana wanafunzi wa vyuo vikuu, wanafunzi wa shule, waumini misikitini na maeneoya ziyara, wanawake wenye mimba na watoto wachanga.Activists Want UN to Recognize Killing of Shias in Afghanistan as Genocide

Serikali ya Afghanistan inalaumiwa kwa kutochukua hatua za kutosha za kuwalinda raia. Watetezi wa haki za binadamu wanataka serikali iwape wanaolengwa haki ya kujiwekea mipango ya usalama iwapo inakabiliwa na changamoto katika kuwalinda.

Hatahivyo vuiongozi wa Kishia nchini Afghanistan wanasisitiza kuwa ni jukumu la serikali kuchukua hatua zozote zinazowezekana kuwalinda.

/3474768

captcha