IQNA

Jeshi la IRGC Iran lalaani hujuma ya kigaidi nchini Afghanistan

18:46 - May 10, 2021
Habari ID: 3473895
TEHRAN (IQNA)0 Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limelaani vikali shambulizi la kigaidi lililolenga shule ya msingi ya Sayed Al-Shuhada mjini Kabul na kuitaja jinai hiyo kuwa ni njama ya Wamarekani ya kutaka kuhuisha ugaidi wa makundi ya kitakfiri na kuvuruga tena amani nchini Afghanistan.

Sehemu moja ya taarifa iliyotolewa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imesema kuwa: Jinai ya Jumamosi Nyeusi huko Kabul na milipuko iliyolenga shule ya wasichana ya Sayed Al-Shuhada katika wilaya ya Dasht-e-Barchi iliyoko magharibi mwa Kabul tena katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, ambayo imepelekea kuuliwa shahidi zaidi ya wasichana 65 na wazazi wao wakiwa katika ibada ya swaumu na kujeruhiwa wengine zaidi ya 160, ni msiba mkubwa uliosababisha simanzi na huzuni kwa Waislamu na wapigaji wa Jihadi nchini Afghanistan.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, hapana shaku kwamba, mtuhumiwa mkuu katika tukio hilo la kuhuzunisha katika kipindi cha sasa ambapo Marekani inadai kuwa inaondoa wanajeshi wake nchini Afghanistan, japo ushahidi unaonyesha kinyume chake, ni Ikulu ya Rais wa Marekani White House ambayo imekuwa ikiwahamisha magaidi wa Daesh kutoka Syria na Iraq na kuwapeleka Afghanistan ili kuendeleza hali ya mchafukoge katika nchi hiyo. 

Taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran imesema: Utawala wa Kigaidi wa Marekani na washirika wake wanapaswa kuhitimisha vita na uhasama wao wa kishetani dhidi ya Umma wa Kiislamu hususan taifa la Afghanistan. Imesema, walimwengu wanaamini kwamba, kuondoka wanajeshi wa Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia kunaweza kurejesha amani na utulivu kwa mataifa ya Waislamu ya eneo hilo. 

Awali msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikuwa amelaani vikali shambulizi la kigaidi lililoa makumi ya watu katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Saeed Khatibzadeh amekosoa vikali hujuma hiyo ya kigaidi iliyolenga raia wa kawaida hususan wanafunzi na ametoa mkono wa pole kwa jamaa za waliouawa na kujeruhiwa katika shambulio hilo la jana Jumamosi.

Aghalabu ya wakazi wa eneo hilo ni Waislamu wa madhehebu ya Shia. Kundi la Taliban limekanusha kuhusika na ugaidi huo na hadi sasa hakuna kundi lolote ambalo limekiri kuhusuka. 

3970648

 

 

https://iqna.ir/en/news/3474676

captcha