IQNA

Rais Rouhani: Wazayuni wauaji hawana uhusiano na dini yoyote ile

23:29 - May 12, 2021
Habari ID: 3473903
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Wazayuni makatili na wauaji hawana uhusiano na dini yoyote ile.

Rais Rouhani amesema hayo leo katika kikao na baraza lake la mawaziri ameashiria jinai za utawala haramu wa Israel na kuuawa wananchhi wasio na hatia wa Palestina na Lebanon na kueleza kuwa, Wazayuni wauaji hawana uhusiano na dini yoyote ile.

Rais Rouhani sambamba na kubainisha kuwa, hii leo Iran takribani imebakia peke yake katika kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina amekikosoa vikali kimya cha mataifa ya Kiislamu na majirani na Palestina.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, kwa nini mataifa makubwa ya Waislamu na yaliyo jirani na Palestina kama Misri, Jordan na nchi nyingine yamemua kunyamazia kimya jinai za utawala haramuu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.

Aidha Rais Rouhani amezungumzia matukio ya Afghanistan ambapo ametoa mkono wa pole kwa taifa hilo kufuatia tukio chungu na la kuhuzunisha la kuwauawa mabinti wa shule na kueleza kwamba, watu ambao wanafanya jinai kama hizi wanachafua jina la Uislamu na kwamba watenda jinai wakuu ni wale walioingilia masuala ya ndani ya Afghanistan.

Rais wa Iran amesema pia kuwa, Israel, Marekani na madola ya Magharibi yameanzisha makundi ya vita vya  niaba ambayo yamekuwa yakifanya jinai katika eneo la Asia Magharibi hususan katika nchi za Afghanistan, Lebanon, Palestina, Syria, Pakistan, Iraq, Yemen, Bahrain na barani Afrika.

3971130

Kishikizo: iran ، rouhani ، quds ، palestina ، israel ، afghansitan
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha