IQNA

Qatar Imetenga dola milioni 500 kwa ajili ya ujenzi mpya wa Ghaza

16:18 - May 27, 2021
Habari ID: 3473950
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema nchi yake itatoa mchango wa dola milioni 500 kwa ajili ya ujenzi mpya wa Ukanda wa Ghaza baada ya vita vya hivi karibuni vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina aktika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taaarifa Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema nchi yake imetenga fedha hizo ikiwa ni katika kuendelea kuwaunga mkono Wapalestina na mikakati ya kuundwa serikali huru ya Palestina.

Katika ujumbe alioutuma kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema Qatar itaendelea kuwaunga mkono Wapalestina ili mgogoro unaowakabili utatuliwe kwa uadilifu na utatuzi huwe uweze kudumu.

Amesema Qatar inaunga mkono uundwaji serikali huru ya Palestina kwa mujibu wa mpango wa amani wa nchi za Kiarbau na marejeo ya kimataifa.

Vita vya mwaka huu vya Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza vilivyoanza Mei 10 na kuendelea kwa siku 12, vilimalizika baada ya kusababisha hasara kubwa za kiuchumi,

Hasara za kiuchumi za vita hivyo tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili, hasara za vita kwa eneo la Ghaza na zile zilizoupata utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika kipindi chote cha siku 12, utawala katili wa Israel ulifanya mashambulizi elfu mbili ya anga dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza. Viongozi wa Gaza wanasema zaidi ya nyumba 1,447 za raia zimeharibiwa kikamilifu katika mashambulizi hayo. Vilevile nyumba nyingine elfu 13 zimepatwa na madhara katika mashambulizi hayo ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Maafisa wa Gaza pia wanasema, jeshi la Israel lilikuwa likilenga kwa makusudi miundombinu na taasisi zote za huduma za kiraia na vituo vya kiuchumi na kwamba mashambulizi ya utawala huo yamesababisha uharibifu mkubwa katika mtandao wa kusambaza maji na barabara za mawasiliano. Raid Jarrar ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Viwanda katika Wizara ya Uchumi ya Ghaza anasema: "Zaidi ya viwanda 50 vimeharibiwa katika mashambulizi ya siku 12 ya Israel. Aidha Kitengo cha Upashaji habari cha serikali ya Palestina katika eneo la Gaza kimetangaza kuwa, mashambulizi ya Israel katika eneo hilo yamesababisha hasara ya dola milioni 322."

/3973994

captcha