IQNA

Ongezeko la asilimia 430 la chuki dhidi ya Uislamu Uingereza

19:51 - May 25, 2021
Habari ID: 3473946
TEHRAN (IQNA)- Ripoti mpya zimebaini kuwa chuki dhidi ya Uislamu yaani Islamophobia imeongezeka nchini Uingereza kwa asilimia 430 kati ya Mei 8-17 ikilinganishwa na wiki moja kabla na ongezeko hilo linatokana na hujuma ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina hasa katika Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Tell MAMA UK, ambayo huchunguza vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu  Uingereza, kuna dalili za wazi kuwa kushadidi hisia za chuki dhidi ya Uislamu nchini humo kumetokana na matukio ya 'Israel na Palestina'.

Tell MAMA inasema imekuwa ikipokea ripoti za kutia wasiwasi kuhusu namna wanafunzi wanavyosumbuliwa shuleni n ahata katika baadhi ya shule waalimu na wasimamizi wamekuwa wakitoa matamshi yaliyojaa chuki dhidi ya wanafunzi Waislamu.

Taasisi hiyo imesema kwa mujibu wa Sheria ya Usawa ya Mwaka 2010, asasi za umma zikiwemo shule zinapaswa kuchukua hatua za kuondoa ubaguzi na kuleta usawa. Aidha Tell MAMA imetaka kuwepo uchunguzi kamili kuhusu vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu sambamba na jamii kupewa mafunzo ili kuwe na ufahamu namna lugha ya kibaguzi inavyowaathiri vibaya wanafunzi na jamii nzima kwa ujumla.

Tarehe 10 mwezi huu wa Mei utawala wa kigaidi wa Israel ulianzisha mashambulizi ya kinyama dhidi ya Ukanda wa Gaza na kuyaendeleza kwa muda wa siku 12. Mamia ya raia wa kawaida hasa wanawake na watoto waliuawa na wengine zaidi ya 2000 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo ambayo pia yamesababisha hasara kubwa kwenye miundomsingi ya kiuchumi na kijamii katika eneo hilo.

3474809/

captcha