IQNA

Balozi wa Syria nchini mjini Tehran

Uhusiano imara wa Iran na Syria ni moja ya mafanikio muhimu ya Mapindui ya Kiislamu kwa watu wa Syria

23:54 - June 03, 2021
Habari ID: 3473976
TEHRAN (IQNA)- Balozi wa Syria nchini mjini Tehran amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa nchi yenye nafasi muhimu zaidi katika eneo na pia katika sera za kimataifa na inahusika katika kuibua mfumo mpya ya kimataifa.

Shafiq Dayoub ameyasema hayo Alhamisi alipohutubu katika Kongamano la Kimataifa la 'Imam Khomeini na Ulimwengu wa Kisasa" ambapo amesema uhusiano imara wa Iran na Syria ni moja ya mafanikio muhimu ya Mapindui ya Kiislamu kwa watu wa Syria. Aidha amesema uhusiano huo unaweza kuwa kigezo cha kuigwa na nchi zingine kuhusu uhusiano ambao umejengeka katika msingi wa maslahi ya pamoja.

Ameongeza kuwa, kukabiliana na madola ya kibeberu ni msingi wa sera za Iran na Syria na kuongeza kuwa: “Sisi hatutasahau namna ambavyo baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ubalozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel mjini Tehran ulifungwa na jengo la ubalozi huo likakabidhiwa Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) huku Iran ikitangaza uungaji mkono wake kamili kwa mapambano ya ukombozi wa Palestina.

Aidha amesema uungaji mkono wa Iran kwa mapambano ya Syria ni kwa maslahi ya malengo matukufu ya Palestina. Balozi Dayoub amesema kuwa Syria katu Katu haitasahau namna ambavyo Iran kwa uongozi wa Ayatullah Khamenei imesimama kidete na watu wa Syria wakati wa kipindi cha vita 10 vya kidhalimu vya magaidi wanaopata himaya ya kigeni dhidi ya nchi hiyo.

 Kongamano la Kimataifa la 'Imam Khomeini na Ulimwengu wa Kisasa" linafanyika leo katika Haram ya Imam Khomeini-Mwenyezi Mungu Amrehemu-Kusini mwa Tehran.

Kwa mujibu wa taarifa kongamano hilo limefanyika kwa mnasaba wa kukumbuka mwaka wa 32 wa kuaga dunia Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya Imam Khomeini (MA) na Mapinduzi ya Kiislamu, Shirika la Habari la Qur'ani la Kimataifa, Taasisi ya Kukusanya na Kuchapisha Fikra za Imam Khomeini (MA) na Idara ya Maadhimisho ya Kuaga Dunia Imam Khomeini (MA).

3975505

Kishikizo: imam khomeini ، iran ، syria
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha