IQNA

Mtazamo

Mtazamo mfupi kuhusu fikra za Imam Khomeini (MA)

20:18 - June 03, 2024
Habari ID: 3478923
IQNA-Leo imetimia mwaka wa 35 tokea alipoaga dunia, Imam Ruhullah Khomeini (Mwenyezi Mungu Amrehemu-MA-) muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Watu wengine wanapokufa, watu husema: Alilazimika kuondoka, maisha yake hayakuwa ya ulimwengu huu. Lakini vifo vingine ni vya uchungu na huzuni, na vingine vinasikitisha. Wanafikra wakubwa  wanapoaga dunia, kuondoka kwao ni tofauti. Imam Khomeini alikuwa shakhsia maalum ambaye Mwenyezi Mungu alimpenda, akamfanya kuwa kiongozi mashuhuri ili watu waweze kufuata njia yake. Tatu Juni inasadifiana na siku ya huzuni, siku ambayo Imam Khomeini alipoaga dunia na kurejea kwa Mola wake. Kabla hatujaendelea napendekeza tusikize aya hizi ya Qur'ani Tukufu ambazi ni aya za 27 hadi 30 za ya Sura Al Fajr......

Ewe nafsi iliyo tua!  Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha.  Basi ingia miongoni mwa waja wangu, Na ingia katika Pepo yangu.

Imam Khomeini (MA), mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alikuwa mtu mashuhuri aliyeanzisha mwamko maarufu zaidi duniani katika zama hizi. Ulikuwa mwamko wa kupinga dhulma na kutafuta uadilifu sambamba na kuutambulisha Uislamu ulimwenguni kuwa dini yenye kumkomboa mwanadamu.

Ruhullah Khomeini alikuwa mujtahid na faqihi mkubwa, na pia mwanafalsafa na mwanairfani. Pamoja na hayo kilichomfanya kuwa kiongozi mkuu wa mapinduzi ya Kiislamu  Iran ni mapambano yake ya dhati na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Hii ni jihadi iliyodumu hadi mwisho wa uhai wake. Alifanikiwa kuuangusha utawala wa kidalimu wa ufalme wa ukoo na kuanzisha serikali yenye msingi ya Kiisalmu na inayozingatia ya Tauhidi."

Leo; tunamkumbuka mtu mashuhuri ambaye ni mwanzilishi wa fikra ya kisiasa na kijamii. Bila shaka, kubakisha hai jina la Imam Khomeini  kunategemea kuelewa misingi yake ya kifikra.

Ufafanuzi kuhusu Uislamu halisi

Imam Khomeini alifanikisha Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979 katika kipindi ambacho mitazamo tofauti  na kinzani kuhusu Uislamu ilikuwa imeibuka duniani.

Lakini rai ya Imam Khomeini ilikuwa kwamba: “Hatuna Uislamu mmoja; Bali, kuna aina tofauti za Uislamu na sio kila Uislamu unaotangazwa ni sahihi; Kuna Uislamu ambao unatumikia  nguvu za kikoloni, ubeberu na ulimwengu wa kibepari, na kuna Uislamu halisi ambao uko katika mwelekeo wa kusaidia mamilioni ya raia, wanyonge, waliokandamizwa na walio chini ya utawala wa ukoloni. Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi chake cha mapambano hususan baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisisitiza kwa uzito na kusisitiza juu ya kutenganisha Uislamu wa kweli na Uislamu potovu.

Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi chake cha mapambano hususan baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisisitiza kwa uzito na kusisitiza juu ya kutenganisha Uislamu wa kweli na Uislamu potovu na uliopotoshwa.

Mbali na kutambulisha vipengele tofauti vya Uislamu sahihi na kupigana dhidi ya dhulma, ukoloni na uistikbari wa kimataifa, Imam alikabiliana na upotoshaji. Katika kuutambulisha Uislamu sahihi wa kweli, alitumia neno “Uislamu Uliotakasika wa Mtume Muhammadi (SAW). Aidha katika kufichua kuhusu Uislamu potovu, alitumia neno “Uislamu wa Marekani” na kusisitiza kwamba “lazima tujaribu kuuteganisha Uislamu halisi uliotakasika na 'Uislamu wa Kimarekani' na tuwaonyeshe waliodhulumiwa uhalisia wa mambo.

Moja ya misingi ya kiitikadi ya Imam Khomeini (MA) ni kuamini ukweli wa ahadi ya Mwenyezi Mungu na kutokuwa na imani na madola yenye kibeberu na kidhalimu duniani. Katika aya ya 7 ya Sura Muhammad, Mwenyezi Mungu anawaambia Waislamu: "Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu."

Mtazamo kuhusu Qur'ani Tukufu

Katika vipindi vyote vya uhai wake, Imam Khomeini alikuwa na imani ya kina kuhusu mafundisho ya Qur’ani na hivyo alichukua maamuzi yake  kwa kutegemea ahadi na msaada wa Mwenyezi Mungu.

Miaka 20 kabla ya kuanza kwa mapambano, yaani tarehe 5 Mei 1954, katika hali ya msukosuko wa kisiasa katika jamii, Imam Khomeini aliandika ujumbe kwa watu wa Iran na wanazuoni wa Kiislamu, ambapo aliwapa nasaha kuhusu ahadi ya Mwenyezi Mungu yaushindi.  Ujumbe huu ulianza na aya ya 46 ya Surah Sabaa isemayo: "Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu"

Kuanzisha harakati ya mwamako kwa ajili Mwenyezi Mungu, harakati ambayo ilimleta Nabii Ibrahim Khalil al-Rahman kwenye nafasi ya ukuruba na Mwenyezi Mungu... Ni mwamko ambao ulipelekea kushindwa  mafirauni kwa fimbo ya Nabii Musa Kalimullah na kuviharibu viti vyao vyote vya katika ufalme wao." ... Mwamko kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ambaye alimpa ushindi Mtume wa Mwisho, Mtume Muhammad SAW, ambaye aliangamiza masanamu yaliyokuwa yamewekwa katika nyumba ya Mwenyezi Mungu na badala yake kuweka msingi wa Tauhidi na Uchamungu…” Naye Imam Khomeini kwa kutegemea imani sawa ya Mitume wa Mwenyezi na kwa kutegemea ahadi na uungaji mkono wa Mwenyezi Mungu, aliweza kufanikisha ushindi Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979.

Imam Khomeini (MA) aliona ni muhimu kuelimisha na kuamsha umma na aliamini kwamba bila ya kuwapa watu ufahamu, hawawezi kutarajiwa kuinuka ili kuulinda na kuutetea Uislamu. Uelimishaji huu wa jamii ni  kwa njia mbili; Elimu ya Uislamu na hukumu zake ili kutambua kuanzishwa kwa serikali ya Kiislamu na mbinu ya pili ni ile ya kufichua jinai na ukandamizaji wa tawala za kiimla na kibeberu na sera zao za chuki dhidi ya Uislamu. Jambo lililomfanya Imam Khomeini asikitike sana  ni kuhusu kupotea kizazi cha vijana na kuliweka mbali na Uislamu tabaka la wasomi wa vyuo vikuu.

Kuhusu nukta hii alisema: “Hapana shaka kwamba Waislamu wakijiongezea maendeleo ya kisiasa na kijamii, wanaweza kuondokana na matatizo mengi  kirahisi na kutatua matatizo ya Umma wa Kiislamu kwa kubadilishana mawazo kutafuta njia muafaka za kusimamia mambo yao. Kwa hivyo, ni wajibu kwa Waislamu wote hasa wasomi wa Kiislamu na wanafunzi wa vyuo vya Kiislamu wasimame dhidi ya sumu inayoenezwa maadui wa Uislamu kwa njia yoyote ile mpaka ibainike kwa kila mtu kwamba Uislamu umekuja kusimamisha serikali ya uadilifu.

Umoja wa Kitaifa

Mtazamo mwingine mkuu wa fikra za Imam Khomeini ni suala la umoja wa kitaifa. Umoja haimaanishi kuwa kuna wazo na msimamo mmoja tu, hali ambayo haifai kamwe. Binadamu wana maoni na fikra tofauti, jambo la muhimu ni kwamba kwa kuwa na tofauti hizi za kimtazamo, wanaweza kuungana pamoja katika kufikia lengo moja. Imam Khomeini aliamini kwamba ni muhimu kupambana na maadui bila ya mgawanyiko na kwa kuwa na umoja wa neno. Iwapo umoja hautakuwepo basi maadui watawashinda Waislamu. Kwa hiyo, katika nasaha zake kwa watu, amesema: “Ni juu ya taifa tukufu la Iran, bila kujali mirengo, kuacha mifarakano na unafiki na malumbano baina yao ili kuweza kukabiliana na adui kwa pamoja... Wazungumzaji katika mihadhara, wasomi na wanafikra wanapaswa kutumia uwezo wao wote kumkatisha tamaa adui wetu mkuu yaani Marekani.

Unyenyekevu wa Imam Khomeini, mwasisi mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ulijulikana sana kwa wote.

Alipokuwa Paris, mwandishi wa habari aliuliza kuhusu maisha yake ya kibinafsi. Imam akajibu: “Maisha yangu ya faragha ni kama maisha ya faragha ya watu wote wa kawaida. Mimi ni mwanafunzi wa kidini kama wanafunzi wengine."

Mwandishi wa Televisheni ya Ujerumani alimuuliza Imam Khomeini kuhusu nguvu na ushawishi wake. Kiongozi huyo wenye busara walijibu: "Mimi ni ndugu na watu wa Iran na ninajiona kuwa mtumishi na askari wao."

Shahidi Raisi, mwanafunzi wa Imam Khomeini

Naan, siku hizi, wakati watu wa Iran wanaomboleza kifo cha kusikitisha cha shahidi Ebrahim Raisi, rais aliykuwa mchamungu na mchapakazi, watu wa dunia walimfahamu zaidi Imam Khomeini na fikra zake kuliko hapo awali. Waliona kwamba mapinduzi ya Khomeini, kwa maana halisi ya neno hili, yako hai na kwamba fikra zake zimekita mizizi. Kujitokeza mamilioni ya  watu wa Iran katika mazishi ya rais wao mwanamapinduzi kuliwakumbusha wengi maombolezo na hisia zao mnamo Juni 1989 wakati wa kifo cha kiongozi wao mshauri, Imam Khomeini. Kwa hakika Seyyed Ebrahim Raisi alikuwa mmoja wa wanafunzi wa kweli wa fikra za Imam Khomeini, ambaye kifo chake, kama kifo cha Imamu wake, kiliumiza nyoyo za Wairani na  Umma wa Kiislamu. Seyyed Ebrahim Raisi" alilikuwa kielelezo za fikra na mitazamo ya  Imam Khomeini.

Kama imamu wake, yeye pia alikuwa mtetezo wa wanyonge na waliodhulumiwa. Kama alivyokuwa Imam Khomeini, alijaribu kwa ushujaa kueneza Uislamu halisi wenye kuzingatia misingi ya uadilifu. Alipambana na matatizo, na kwa njia hiyo hiyo, alijitolea muhanga maisha yake na hatimaye alifufa shahidi  kujiunga na Imam wake.

Habari zinazohusiana
Kishikizo: imam khomeini
captcha