IQNA

Mjumbe wa Jihad Islami ya Palestina nchini Iran atembelea ofisi za IQNA

21:18 - January 21, 2021
Habari ID: 3473579
TEHRAN (IQNA)- Mjumbe wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina nchini Iran Nasser Abu Shariff ametembelea ofisi za Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) hapa mjini Tehran.

Afisa huyo wa Jihad Islami ametembelea vitengo mbali mbalia vya IQNA Jumatano na kufahamishwa kuhusu shughuli za shirika hilo la habari.

Abu Sharif alikutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa IQNA, ambaye pia ni kaimu mkuu wa Akademia ya Harakati za Qur’ani nchini Iran Mohammad Hussein Hassani.

Abu Sharif amesisitiza kuwa harakati zote za Waislamu zinapaswa kuwa kwa msingi wa mafundisho ya Qur’ani Tukufu. Amsema kuwa huisoma Qur’ani Tukufu mara kwa mara na hujitahidi kufahamu na kufasiri mafundisho yake ikiwa ni pamoja na mitazamo ya Qur’ani kuhusu siasa.

Ametoa mfano na kusema analaani hatua ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel kwa kuzingatia aya za Qur’ani Tukufu.

Mwanadiplomasia huyo wa Jihad Islami ametoa shukrani zake za dhati kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na jitihada zake za kuhuisha adhama ya Umma wa Kiislamu na kuufanya uwe umma bora na uliostawi zaidi duniani.

Aidha amesema Iran ni kituovu cha mradi wa mwamako wa Kiislamu na kuongeza kuwa: “Si tu kuwa sisi ni waitifaki wa Iran katika mradi huu bali sisi ni sehemu ya mradi huu.”

Kwa upande wake Bw. Mohammad Hussein Hassani amefafanua kuhusu kazi za IQNA na Akademia ya Harakati za Qur’ani nchini Iran. Amesema taasisi hizo mbili zinafungamana na kustawisha harakati za muqawama na mapambano ya Kiislamu sambamba na kutetea heshima ya Waislamu duniani kote.

رد نشود؛ بازدید نماینده جنبش جهاد اسلامی فلسطین در تهران از ایکنا
 
3473761/

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha