IQNA

Israel yakiuka mapatano ya usitishaji vita, yahujumu Ghaza

19:53 - July 02, 2021
Habari ID: 3474064
TEHRAN (IQNA)- Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimeshambulia maeneo ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukanda wa Ghaza na hivyo kukiuka mapatano ya hivi karibuni ya usitishwaji vita.

Utawala wa Kizayuni wa Israel umetekeleza hujuma hiyo kwa kisingizio kuwa baloni zenye mabomu na kudai kwambe kituo cha Hamas kilicholengwa kilikuwa kinaunda silaha.

Mwezi Mei utawala haramu wa Israel ulianzisha vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza na kuwaua Wapalestina zaidi ya 250 wakiwemo wanawake na watoto wengie. Utawala huo ghasibu ulilazimishwa kutangaza usitishaji vita baada ya harakati za ukombozi wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza kuvurumisha makombora karibu 4000 kuelekea katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa  jina la Israel.

Hamas imeutahadharsiha utawala dhalimu wa Israel kuhusu vitendo hivyo vya ukiukwaji mapatano ya usitishaji vita kwa kuukumbusha utawala huo kuhusu pigo ambalo ulipata katika vita hivyo vya siku 12 vya mwezi Mei ambavyo ni maarufu kama  vita vya 'Upanga wa Quds'.

3475118

Kishikizo: ghaza palestina israel quds
captcha