IQNA

18:40 - June 30, 2021
Habari ID: 3474057
TEHRAN (IQNA)- Viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na Harakati ya Jihadi Islami ya Palestina wamekutana na kusisitiza kuhusu ulazima wa kuimarisha na kudumisha umoja baina ya Wapalestina.

Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas na Katibu Mkuu wa Jihad Islami Ziyad al-Nakhala wamesisitiza nukta hiyo walipokutana mjini Beirut.

Viongozi hao walijadili njia za kutumia ipasavyo mafanikio ya hivi karibuni ya  'Oparesheni ya Upanga wa Quds' dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel mwezi Mei katika Ukanda wa Ghaza na haja ya Wapalestina kuwa na msimamo wakati wa kukabiliana na changamoto zilizopo.

Haniya aliwasili Beirut Jumapili kwa lengo la kufanya mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu Lebanon na viongozi wa harakati za muqawama wenye makao yao Beirut akiwemo Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah.

Ujumbe huo wa Hamas awali ulitembelea Morocco na Mauritania kabla ya kuwasili Lebanon.

3981203

 

Kishikizo: hamas ، hizbullah ، jihad islami ، haniya ، nakhala
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: